Skip to main content

KWA NINI SIIAMINI BIBLIA

                                                   
Karibuni sana wasomaji wetu wa tovuti hii ambayo ni maalumu kabisa kwa kupanua wigo wa kuielewa biblia ilivyo na uhalisia unaoendelea katika dunia hii.Hii ni makala ya kwanza kabisa kwa wasomaji  wetu wa tovuti hii katika mfululizo wa matoleo yatakayo endelea.Kwa kuwa yanayoandikwa humu  ni mambo yaliopo kwenye biblia na kwa kuwa wasomaji wa makala hii ni wasomaji wa biblia hiyohiyo, sitaki kumaanisha ninawakwaza watu kwa kuidadisi biblia,bali ni sehemu ya kupata changamoto, elimu na kukumbushana kuisoma biblia na kuielewa.Pia ninazitambua juhudi za waandishi wa biblia kuchangia kueneza neno la mungu ambalo tunalo sasa na kuliishi wamefanya kazi kubwa sana.Bila kuwasahau wahubiri wetu wa neno la mungu maaskofu, mapadre wachungaji mbalimbali na wazee wa makanisa mbalimbali duniani kwote wamefanya na wanafanya kazi kubwa ya kueneza injili kwetu natambua mchango wao ambao umeifanya dunia kuwa tulivu ,na watu kuwa wastaarabu na kuwa na ujuzi mbalimbali wa kiroho na hata wa kiuchumi,utamaduni na kisiasa kwenye jamii zetu.Mimi si wa kwanza kuidadisi biblia na kufikia hatua ya kusema siiamini biblia bali wapo wengi tu duniani labda huenda hatujaielewa bado kuwa inamaanisha nini mpaka sasa.Nipo tayari kuamini uhalisia wowote unaoendana na maandiko.Nipo tayari vilevile kupokea ushahidi wa maandiko ya biblia na uhalisia uliopo sasa unaoendelea.Simzuii mtu kutoa maoni yake ila yaendane na maandiko ya biblia.Sikatai ushauri kutoka kwa yeyote Yule ijapokuwa wapo watakaopingana na hoja nitakazoziweka hapo chini.Haitakuwa busara kutoa lugha za matusi au lugha zinazofanana na matusi kwa sababu lengo kubwa ni kupeana elimu juu ya biblia kutokana na mfululizo wa hoja nilizonazo na ambazo zipo kwenye biblia hiyohiyo.Kinyume na hapo utakuwa unagombana na biblia yenyewe.
Nimekuwa nikiiamini biblia na bado ninaifurahia kama fasihi (huenda siisomi au ninaisoma sana kuliko wengi marafiki wakristu wenzangu) lakini siitumaini kama ni kitabu chenye nguvu ya kimungu kwa mtazamo wa kibinadamu tulionao. Kwa nini? Majibu ni marefu sana na ni magumu kidogo hivyo sitakuchosha sana wewe msomaji wa makala hii.
“BIBLIA ni neno la MUNGU”.Hili wazo tunalo na tunaishi nalo kila siku.Tena tunaenda mbali na kusema “MUNGU aliandika biblia”.Na tukiendelea tukisema “KITABU CHA MUNGU”Huu ni ufahamu wa hali ya juu na utaalamu wa kuwapa watu moyo,matumaini na faraja kipindi cha taabu nyingi wakati wa kukabiliana na mambo yasiyojulikana.Wakristu,wayahudi,waislamu,wamomoni,wahindu,wabudha na wengineo ambao wanadai kuwa na maandiko yenye nguvu za kimungu wanashuhudia haya kila siku.
Jambo hili nikajikuta nashindwa kulikalia kimya.Na ninajikuta ninachagua njia niliyonayo sasa ya kutokuwa na imani na biblia kama ni neno la mungu.Na nitashangaa kama shetani ndiye aliyenidanganya kuyasema haya au la.
Tunaposoma biblia maranyingi tunakuwa na mawazo kati ya haya mawili:
(i)Biblia inapumzi ya mungu angalau kwa kiasi Fulani
(ii)Biblia imeandikwa na binadamu tu kwa utashi wake bila nguvu ya mungu ndani yake
Ninavyoona mimi kwamba kama mtu akichunguza biblia kwa usahihi,atachagua namba mbili
(a)Biblia imesheheni kauli nyingi sana ambazo zinapingana zenyewe kwa zenyewe na zinatatiza
Ilishawahitokea kwamba niliwahi kutaka hadharani kuwa biblia ni sahihi,inamsimamo , haidanganyi na haina utata hata kama imeandikwa na waandisho zaidi ya 40 na hata kama imeandikwa zaidi  ya miaka 1500.Inasimulia habari moja moja na ni zilezile na ndio utamaduni wa kikristu ambao umeingia kwenye utamaduni wa kiprotestant uliokithiri kwa sasa.Kuna wachambuzi mbalimbali wa biblia akiwemo huyu kutoka ISRAEL (UYAHUDI) anaitwa :
MICHAEL KARASIK anasema “Sehemu mbalimbali za biblia zimeandikwa vipindi tofauti,kwa mtindo tofauti na watu tofauti wenyemitazamo tofauti.Na kwamba dunia ni kama yetu tu ilikuwepo na watu walitofautiana kwa kelele nyingi maranyingi kuhusu siasa,na kuhusu dini.Tofauti hizi pamoja na zingine ambazo wakati mwingine za binafsi sana ndio zote zinazopatikana leo zilizokusanywa na ndizo tunazoziita biblia”
Huyu ni msomi wa kiyahudi wa biblia.
Mwingine ni  JAQUES BERLINABLAU ambaye ni mwandishi wa fasihi ya wahebrania wa kale anasema kama ifuatavyo   “Miongoni mwa changamoto kubwa sana ambazo mhadhiri wa biblia chuoni anakabiliana nazo ni kudhaniwa kutofikiri kuwa biblia ni kitabu cha kisasa.
Wengine ni wachambuzi wa vitabu vya deuterokanoni ambao ni Profesa Ronald J. Alen na Joseph katika kitabu chao wanasema “injili moja masikio mengi”waandishi wa biblia wanatofautiana.
Kwa mfano wadeuterokanoni  wana wanachukulia kwamba utiifu unazaa ustawi na mafanikio wakati jeuri  inakaribisha laana.Lakini kitabu cha AYUBU kinasema kwamba “sio lazima”

Wasomaji wanashauriwa kwenye kitabu cha 1 PETRO  kwamba kuwa watiifu kwa watawala kwa kuwa watawala ni wawakilishi wa mungu.Lakini kitabu cha ufunuo kinatazama kama dola ya kirumi ni kifaa cha shetani.....itaendelea toleo lijalo.

Comments

Popular posts from this blog

GO FURTHER